Thursday, 14 December 2017

Serikali yashauriwa kuongeza huduma za pamoja kwa wahanga wa ukatili

SERIKALI imetakiwa kuongeza idadi ya vituo vinavyotoa huduma ya pamoja kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ ili kuwasaidia waathirika wa matukio hayo.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi –CRC, Bi. Gladness Munuo kilichopo chini ya TAMWA, alipokuwa akiwasilisha mada kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanahabari juu ya huduma za ‘One Stop Center’.
Bi. Gladness Munuo alisema huduma ya pamoja kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia zinaumuhimu mkubwa kwa jamii, kwani mbali ya kuwahudumia wahusika zinachochea elimu ya uelewa kwa jamii juu ya matukio ya ukatili na namna ya kudhibiti.


Alisema licha ya umuhimu huo, mahitaji ya huduma hizo kwa jamii ni makubwa hivyo kuna kila sababu ya serikali kujenga vituo vya kutosha vinavyotoa huduma hizo ili kusogeza huduma jirani na waathirika.
Aidha alisema Novemba 14 hadi 16 kituo cha CRC kilifanya majaribio ya utoaji huduma kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia, hasa kwa akina mama na watoto jambo ambalo lilibaini uitaji mkubwa wa huduma kwa jamii.
Hadi sasa kwa Tanzania nzima kuna idadi ya vituo vinne pekee vya huduma ya pamoja kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’, ambapo vyote vipo jijini Dar es Salaam licha ya uhitaji katika maeneo mengine anuai.
Kituo cha Usuluhisihi cha CRC (Crisis Resolving Centre) ni Shirika lisilo la kiserikali ambalo lililoanzishwa mwaka 2007 chini ya TAMWA, kwa ajili ya kutetea haki za binadamu kwa kulinda haki na ustawi wa watoto na wanawake.

No comments:

Post a Comment

CRC YATOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI MAKUMBUSHO

Kituo cha usuluhishi na Upatnishi  (Crisis Resolving Center – CRC) kimetoa huduma ya siku mbili inayojulikana kama huduma ya mkono kwa mkono...