Saturday 30 December 2017

Crisis Resolving Centre (CRC) was among the organisation funded by WFT within this year 2017 whereby CRC implemented a project titled Women Visibility! The project complented with successful.Live long WFT.


Women Fund Tanzani (WFT) on 30th December, 2017 hold a one day meeting specific on feedback meeting with the Stakeholders (NGO) funded by WFT for the year 2017.



Rose Njilo Director Mumitie Women Organization (MWO)

Thursday 14 December 2017

JE, MWANANCHI UNAITAJI HUDUMA HIZI…!


JE, UNAITAJI HUDUMA HIZI…!
-MSAADA WA KISHERIA
-USHAURI NASIHI
-HUDUMA ZA DAWATI LA JINSIA (CHINI YA JESHI LA POLISI)
KITUO CHA USULUHISHI, CRC KINAKULETEA HUDUMA HIZO BORA ZA PAMOJA NA BURE. NA KWA WAKAZI WA KAWE JIJINI DAR ES SALAAM HUDUMA HIZI ZITAKUWA MTAANI KWAKO, KUANZIA DESEMBA 14-15, 2017. MAHALI NI OFISI YA MTENDAJI WA KATA YA KAWE (KAWE-KANISANI). KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA TISA ALASIRI.
KWA MAWASILIANO TUPIGIE: 0762625523, KWA MSAADA WA USHAURI ZAIDI.

Wananchi Saranga wavutiwa na huduma za ‘One Stop Centre’




BAADHI ya wananchi wanaoishi Kata ya Saranga eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam wamejitokeza kupata huduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.
Huduma hiyo iliyoanza kutolewa Desemba 11 na Kituo cha Usuluhishi –CRC, kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) imelenga kusogeza karibu na wananchi huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo.
Huduma zilizotolewa ni pamoja na msaada wa kisheria kwa waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, Ushauri Unasihi na Dawati la Jinsia linalohudumiwa na Jeshi la Polisi. Wakizungumza baadhi ya wananchi waliopatiwa huduma kituoni hapo walisema wanafurahishwa na huduma hizo muhimu kutolewa eneo moja jambo ambalo linawapunguzia mzigo na urasimu wanapoziitaji.
“Mimi nawashukuru sana waliotuletea huduma hizi (CRC) jirani, hii inatupunguzia mzigo kwa kweli kuna mlolongo mkubwa sana unapozifuatilia maeneo mengine, tungependa zitolewe siku zote kama leo, nadhani vitendo hivi vingepungua,” alisema Ally Mpate akizungumza mara baada ya kupata huduma.
Kwa upande wake Bi. Salome Mlimbo alisema wapo baadhi ya watu wanaishi ndani ya vitendo vya unjanyasaji lakini wanashindwa kujitokeza kutokana na umbali na urasimu uliopo katika kupata huduma hizo, hivyo kushauri zisogezwe jirani na pamoja.
Hivi karibuni Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi –CRC, Bi. Gladness Munuo kilichopo chini ya TAMWA, aliishauri Serikali kuongeza idadi ya vituo vinavyotoa huduma ya pamoja kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ ili kuwasaidia waathirika wa matukio hayo.



Serikali yashauriwa kuongeza huduma za pamoja kwa wahanga wa ukatili

SERIKALI imetakiwa kuongeza idadi ya vituo vinavyotoa huduma ya pamoja kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ ili kuwasaidia waathirika wa matukio hayo.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi –CRC, Bi. Gladness Munuo kilichopo chini ya TAMWA, alipokuwa akiwasilisha mada kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanahabari juu ya huduma za ‘One Stop Center’.
Bi. Gladness Munuo alisema huduma ya pamoja kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia zinaumuhimu mkubwa kwa jamii, kwani mbali ya kuwahudumia wahusika zinachochea elimu ya uelewa kwa jamii juu ya matukio ya ukatili na namna ya kudhibiti.


Alisema licha ya umuhimu huo, mahitaji ya huduma hizo kwa jamii ni makubwa hivyo kuna kila sababu ya serikali kujenga vituo vya kutosha vinavyotoa huduma hizo ili kusogeza huduma jirani na waathirika.
Aidha alisema Novemba 14 hadi 16 kituo cha CRC kilifanya majaribio ya utoaji huduma kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia, hasa kwa akina mama na watoto jambo ambalo lilibaini uitaji mkubwa wa huduma kwa jamii.
Hadi sasa kwa Tanzania nzima kuna idadi ya vituo vinne pekee vya huduma ya pamoja kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’, ambapo vyote vipo jijini Dar es Salaam licha ya uhitaji katika maeneo mengine anuai.
Kituo cha Usuluhisihi cha CRC (Crisis Resolving Centre) ni Shirika lisilo la kiserikali ambalo lililoanzishwa mwaka 2007 chini ya TAMWA, kwa ajili ya kutetea haki za binadamu kwa kulinda haki na ustawi wa watoto na wanawake.

KITUO CHA CRC CHAWANOA WANAHABARI HUDUMA ZA 'OSC'



CRC YATOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI MAKUMBUSHO

Kituo cha usuluhishi na Upatnishi  (Crisis Resolving Center – CRC) kimetoa huduma ya siku mbili inayojulikana kama huduma ya mkono kwa mkono...