Thursday 17 May 2018

CRC YATOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI MAKUMBUSHO

Kituo cha usuluhishi na Upatnishi (Crisis Resolving Center – CRC) kimetoa huduma ya siku mbili inayojulikana kama huduma ya mkono kwa mkono au ‘one stop center’.

Huduma hiyo ilianza May 15 na kumalizika May 16 ambapo huduma za msaada wa kisheria na elimu ya kisheria juu ya kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia zilitolewa. 

Wananchi waliojitokeza walisaidiwa katika kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo na uelewa wa elimu ya kisheria katika kutambua haki zao na kuwaona wataalam mara wanapokumbwa na matukio yanayoitaji msaada wa kisheria.

CRC chini ya ufadhili wa Shirika la Legal Service Facility (LSF) wamejipanga kutoa huduma za 'one stop center' katika kata za Kawe na Saranga zote za jijini Dar es Salaam.






Tuesday 8 May 2018

CRC HOST ITS 8th AGM SUCCESSFUL ON 5th May 2018

CRC Members in group photo during its 8th Annual General Meeting (AGM) held on 5th May 2018 at TAMWA Conference Hall, at Sinza mori, Dar es Salaam.

Wednesday 2 May 2018

CRC AGM ON 5th May 2018

On 5th May, 2018 Crisis Resolving Centre (CRC) is going to host a 7th Annual General Meeting (AGM). That important event shall be done at TAMWA Conference Hall-Sinza Mori, DSM. The AGM is a supreme organ, therefore all members are invited to attend.

Saturday 28 April 2018

CRC YAKUTANA NA WASAIDIZI WA KISHERIA NA MAAFISA USTAWI WASAIDIZI


Afisa mradi kutoka kituo cha usuluhishi (Crisis Resolving Center - CRC) Bi Suzana Charles Mwaitenda akiendesha mkutano na wadau wa mradi wa uwezeshwaji wa masuala ya kisheria unaofadhiliwa na shirika la msaada wa kisheria ( Legal Service Facility - LSF).
Mkutano huo uliwahusisha wasaidizi wa kisheria na afisa ustawi wasaidizi kujadili maendeleo ya mradi ulipofikia, changamoto na mafanikio.

Tuesday 13 February 2018

CRC YATOA HUDUMA ZA MKONO KWA MKONO(‘ONE STOP CENTER’) KWA WAKAZI WA MWANANYAMALA KATA YA MUKUMBUSHO DAR ES SALAAM.


Kituo cha Usuluhishi na Upatanishi (Crisis Resolving Center – CRC) kimetoa huduma ya siku mbili inayojulikana kama huduma ya mkono kwa mkono au ‘one stope center’. Huduma hii ilianza jana tarehe 12 na itamalizika leo tarehe 13 ambapo wahanga wa ukatili wa kijinsia  wanapatiwa bure huduma za pamoja  kutoka kwa Wanasheria, Polisi, Madaktari na Afisa ustawi wa jamii.


Akitoa tathmini fupi kwa huduma iliyotolewa jana kwa wakazi wa Mwananyamala, Afisa ustawi wa jamii wa kituo cha usuluhishi na upatanishi (CRC) Bi Violeth Chonya alisema, muitikio wa wananchi waliojitokeza kupata huduma za pamoja ni mkubwa, ambapo jumla ya kesi 31 zilisikilizwa na kufikia hatua mbalimbali huku kesi 2 za matuzo kwa watoto zikitatuliwa baada ya kukutanishwa pande mbili za wazazi na kufikia muafaka juu ya mvutano baina yao.

Bi. Violeth alisema kuwa muitikio mkubwa wa wananchi unaonyesha uhitaji mkubwa wa huduma hii kwa jamii huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi leo amabapo hii inaendelea kutolewa kwa siku ya pili na ya mwisho kwa eneo la Mwananyamala.








Saturday 30 December 2017

Crisis Resolving Centre (CRC) was among the organisation funded by WFT within this year 2017 whereby CRC implemented a project titled Women Visibility! The project complented with successful.Live long WFT.


Women Fund Tanzani (WFT) on 30th December, 2017 hold a one day meeting specific on feedback meeting with the Stakeholders (NGO) funded by WFT for the year 2017.



Rose Njilo Director Mumitie Women Organization (MWO)

CRC YATOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI MAKUMBUSHO

Kituo cha usuluhishi na Upatnishi  (Crisis Resolving Center – CRC) kimetoa huduma ya siku mbili inayojulikana kama huduma ya mkono kwa mkono...