Thursday, 17 May 2018

CRC YATOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI MAKUMBUSHO

Kituo cha usuluhishi na Upatnishi (Crisis Resolving Center – CRC) kimetoa huduma ya siku mbili inayojulikana kama huduma ya mkono kwa mkono au ‘one stop center’.

Huduma hiyo ilianza May 15 na kumalizika May 16 ambapo huduma za msaada wa kisheria na elimu ya kisheria juu ya kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia zilitolewa. 

Wananchi waliojitokeza walisaidiwa katika kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo na uelewa wa elimu ya kisheria katika kutambua haki zao na kuwaona wataalam mara wanapokumbwa na matukio yanayoitaji msaada wa kisheria.

CRC chini ya ufadhili wa Shirika la Legal Service Facility (LSF) wamejipanga kutoa huduma za 'one stop center' katika kata za Kawe na Saranga zote za jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a comment

CRC YATOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI MAKUMBUSHO

Kituo cha usuluhishi na Upatnishi  (Crisis Resolving Center – CRC) kimetoa huduma ya siku mbili inayojulikana kama huduma ya mkono kwa mkono...