Tuesday, 13 February 2018

CRC YATOA HUDUMA ZA MKONO KWA MKONO(‘ONE STOP CENTER’) KWA WAKAZI WA MWANANYAMALA KATA YA MUKUMBUSHO DAR ES SALAAM.


Kituo cha Usuluhishi na Upatanishi (Crisis Resolving Center – CRC) kimetoa huduma ya siku mbili inayojulikana kama huduma ya mkono kwa mkono au ‘one stope center’. Huduma hii ilianza jana tarehe 12 na itamalizika leo tarehe 13 ambapo wahanga wa ukatili wa kijinsia  wanapatiwa bure huduma za pamoja  kutoka kwa Wanasheria, Polisi, Madaktari na Afisa ustawi wa jamii.


Akitoa tathmini fupi kwa huduma iliyotolewa jana kwa wakazi wa Mwananyamala, Afisa ustawi wa jamii wa kituo cha usuluhishi na upatanishi (CRC) Bi Violeth Chonya alisema, muitikio wa wananchi waliojitokeza kupata huduma za pamoja ni mkubwa, ambapo jumla ya kesi 31 zilisikilizwa na kufikia hatua mbalimbali huku kesi 2 za matuzo kwa watoto zikitatuliwa baada ya kukutanishwa pande mbili za wazazi na kufikia muafaka juu ya mvutano baina yao.

Bi. Violeth alisema kuwa muitikio mkubwa wa wananchi unaonyesha uhitaji mkubwa wa huduma hii kwa jamii huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi leo amabapo hii inaendelea kutolewa kwa siku ya pili na ya mwisho kwa eneo la Mwananyamala.
No comments:

Post a comment

CRC YATOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI MAKUMBUSHO

Kituo cha usuluhishi na Upatnishi  (Crisis Resolving Center – CRC) kimetoa huduma ya siku mbili inayojulikana kama huduma ya mkono kwa mkono...