Wednesday, 25 October 2017

      Bi Huruka: Ni mjasiriamali ambaye anaishi na virusi vya ukimwi  kwa muda wa miaka 27, anatengeneza batiki mwenyewe na kuuza sehemu mbalimbali. Pia ameweza kumsomesha mtoto wake mpaka ngazi ya chuokikuu kupitia ujasiriamali wake.
Bi Huruka  (pichani kulia) alipofanya mahojiano na mwandishi wa habari.

     Janeth Mawinza: Ni mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama WAJIKI (Wanawake katika jitihada za kimaendeleo), yeye ni mwanaharakati binafi ambaye anapinga masuala ya ukatili wa kijinsia katika jamii inayomzunguka. Masuala ya ukatili anayopambana nayo ni pamoja na ubakaji, ulawiti, vipigo, udhalilishwaji n.k. Ni mtu anayechulua hatua za haraka panapotokea ukatili wa kijinsia katika eneo lake. Pia anafanya kazi karibu na kituo cha usuluhishi kwa kufuatilia kesi za ukatili wa kijinsia Mahakamani, Polisi, Ustawi wa jamii n.k 

Janeth Mawinza: Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama WAJIKI (Wanawake katika jitihada za kimaendeleo)


Mkurugenzi wa TAMWA – Edda Sanga akifungua mkutano  wa wadau ambao ni wanawake 6 wa mfano walioshiriki katika kazi mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kijamii na kuleta matokeo katika jamii.

Mkurugenzi wa TAMWA – Edda Sanga


CRC YATOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI MAKUMBUSHO

Kituo cha usuluhishi na Upatnishi  (Crisis Resolving Center – CRC) kimetoa huduma ya siku mbili inayojulikana kama huduma ya mkono kwa mkono...